|     Tel: +255 (0) 773 277 681 | Email: info@zari.or.tz | Miwani Road, Kizimbani,Zanzibar
ZARI Header Image
UDHIBITI WA VIWAVI JESHI ZANZIBAR-February 2019

UDHIBITI WA VIWAVI JESHI ZANZIBAR-February 2019

SHIRIKA LA CHAKULA NA KILIMO (FAO) LIMEFANYA MAFUNZO YA UDHIBITI WA VIWAZI JESHI VAMIZI KWA WATAALAMU NA MAAFISA WA KITENGO CHA UTIBABU WA MIMEA WA UNGUJA NA PEMBA AKIFUNGUA MAFUNZO HAYO MKURUGENZI WA IDARA YA KILIMO NDUGU MOHAMED KHAMIS RASHID AMESEMA VIWAVI JESHI NI WADUDU WANAADHIRI KWA KIASI KIKUBWA MAZAO YA MPUNGA NA MAHINDI AMBAYO HUREJESHA NYUMA JITIHADA ZA MKULIMA SAMBAMBA NA KUMKOSESHA MKULIMA MAZAO KWA AJILI YA CHAKULA NA BIASHARA. AKIWASILISHA MADA MWAKILISHI WA SHIRIKA LA CHAKULA NA KILIMO (FAO) NDUGU MUSHOBAZI BAITANI AMEELEZA KUWA NJIA INAYOFAA KUWADHIBITI VIWAVI JESHI NI KWA WATAALAMU WA KILIMO KUFANYA UKAGUZI WA MASHAMBA MARA KWA MARA ILI KUGUNDUA KAMA KUNA DALILI ZA AWALI ZA KUWEPO KWA VIWAVI JESHI NA KUWEZA KUWEPUKA HASARA KWA WAKULIMA KUKOSA MAZAO YAO.

Close Menu